TIBU - UTI

 NAMNA YA KUTIBU NA KUTATUA TATIZO LA UTI/UTI SUGU.

My Views


MAANA: UTI Ni ugonjwa unaoathili sehemu za siri za watu, ambao huanzia kwenye mfumo wa haja mdogo na baadae mifumo ya sehemu za siri na za uzazi za wanaume na wanawake baada ya kupata maambukizi ya bacteria mbalimbali wasababishao UTI.

Sababu za Maambukizi

UTI husababishwa na bakteria wengi tofauti ambao huathiri sehemu za haja ndogo japo huweza sambaa Hadi sehemu za siri za mgonjwa mwenye ugonjwa huo hasa Kama ni UTI kali Sana au Sugu., 

Vipimo na uchunguzi:

Vipimo na uchunguzi wa ugonjwa wa UTI hufanyika kwa kuangalia vyote dalili za UTI na vipimo vya Maabara, mfano, Kipimo cha MKOJO, na maumivu sehemu za njia ya mkojo ni moja kipimo na dalili za ugonjwa huo.

Kwa hiyo ikiwa ukipata dallili zifuatazo fika kituo cha huduma kupima na kupata matibabu au kufanya uchunguzi zaidi.


DALILI ZA UGONJWA WA UTI

Mgonjwa au mtu mwenye ugonjwa wa UTI atapata moja ya dalili zifuatazo au zote.

1.Maumivu wakati wa kukojoa.

2.Muwasho sehemu za siri au njia ya mkojo.

3.Maumivu chini ya Kitovu.

4.Maumivu (yasio ya kawaida) wakati wa kufanya tendo la Ndoa. n.k


*Kumbuka dalili hizo zinaweza kuonekana kwa ugonjwa wa UTI au zikaambatana na dalili zingine za magonjwa mengine kama kaswende, gono, kichocho n.k

Kwa hiyo ni vizuri kufika katika kituo cha kutolea huduma za afya kujua utofauti wa dalili zenyewe na UTI na kupata matibabu mapema.


MATIBABU YA UGONJWA WA UTI.

Baada ya kupima na kuonekana una ugonjwa wa UTI kutoka katika kituo cha kutolea huduma, kuna mambo muhimu ambayo mtu anaeumwa UTI atatakiwa kuyafanya na kuyafuata ili kuhakikisha matibabu kamilifu ya ugonjwa wa UTI.


MATIBABU KAMIRIFU YA UTI.

  1. Kutumia dawa ulizopewa katika kituo cha kutolea huduma.
  2. Kuhakikisha Afya ya mwili na usafi.
  3. KuiishiAfya ya mwili kikamili kila hatua.
  4. Kutumia matunda, Maji ya kutosha na vyakula vyenye kiwango kingi cha maji.


HATUA ZA KUFUATA

1.Nenda katika kituo cha kutolea huduma za Afya na kama ukiwa na UTI.

2. Kusanya chupi na au boxer zotev ulizofua na ambazo haujazifua zifue tena vizuri kwa sabuni na maji safi, unaweza pia kufulia maji ya moto.

3.Zikaushe vizuri kwenye jua kali kuanzia asubuhi hadi jioni na uzitoe kabla jua halijazama na zikaanza kuweka unyevu, zinyooshe nguo hizo na pasi, kwa wale ambao jua halipo mda mrefu mnaweza kunyoosha tu kwa pasi baada ya kuzikausha

4. Siku inayofuata tumia dawa ulizoambiwa na daktali na uvae chupi au boxa safi iliyokaushwa juani au iliyokaushwa juani na kunyooshwa.

5. Haikikisha unabadilisha chupi zako mara 3 au 4 kwa siku pia boxa kwa wanaume ubadilishe zaidi ya mara 3 kwa siku, ikiwa mtaweza kubadilisha nguo hizo za ndani zaidi ya mara 4 kwa siku nayo ni sawa ndio inayotakiwa.

6. Hakikisha kila wakati kabla ya kubadili chupi au boxa iliyo nyooshwa na au iliyopigwa pasi, uhakikishe unajisafisha vizuri na kukausha sehemu za siri kwa maji safi na nguo au taulo uliyotumia kujikaushia uianike juani.

7.Usianike Chupi au boxer au nguo ya ndani , ndani ya nyumba baada ya kuifua usiku au mchana, hasa Kama huwezi kuzinyoosha kwa pasi.

8. Hakikisha unatumia maji safi na salama ya kutosha wakati ukiendelea na matibabu na hata ukisha pina ugonjwa wa UTI. kuanzia lita 2 na kuendelea kwa siku.

9. Usiwe na unyevyunyevu sehemu za siri kwa sababu bacteria wa UTI na magonjwa ya sehemu za siri wanapenda Sana na wanazilana zaidi kwenye mazingira Kama hayo sehemu hizi.

10. Inashauliwa kulala bila nguo ya ndani wakati wa usiku kwa sababu joto maeneo ya siri huongeza kuzaliana kwa bakteria.

11. Hakikisha unakula matunda yenye maji mengi Kama matikiti, matango, nashauli aina hiyo ya matunda kwa maana yanasaidia sana kusafisha ini, figo na njia ya mkojo.

12. Ishi maisha haya na kama umeoa au umeolewa lazima mtibiwe wote, au Kama mnamahusiano ya kimapenzi na mpezi wako kwa maana kwamba mnashiliki tendo la Ndoa lazima mpate matibabu nyote.

13. Ukiweza wakati wa matibabu Kama wiki 1 au 2 ivi mnaweza acha kufanya mapenzi Hadi baada ya mda huo wa matibabu.

14. Ni jambo jema kwa kila jambo la ki afya kupima na kuangalia tena kwa vipimo kuona maendeleo ya afya kuona kua umepona au imekaaje baada ya matibabu.

15. Ili kuhakikisha matibabu kamilifu ni vyema kuangalia sababu zingine za magonjwa ya njia ya mkojo au njia ya sehemu za siri.


ASANTE KWA KUSOMA, NAAMINI MAKALA HII IMEKUA YA MUHIMU SANA KWAKO NA AFYA YAKO.

Tafadhari tutumie maoni yako Kama makali hii umeipenda na inataarifa muhimu kwako na pia baada ya kufuata ushauri na maelekezo haya umepata suruhu ambalo makala hii ililenga kukupatia.

Maoni yako yatasaidia kutufanya tuaminiwe zaidi na zaidi Sana kuweza kuwasaidia wengine wenye uhitaji kwa muda muafaka.

Tuma maoni yako kwenda kwenye Email. embrooos@gmail.com

Or whatsapp +255688707864

Tuna vitabu vingine na topiki zingine Kama.πŸ‘‡

* MAUMIVU NAPOKUA NAFANYA MAPENZI-PAIN WHEN HAVING SEX.

* KWANINI NAPATA MAUMIVU MAKALI NAPOFANYA TENDO LA NDOA - WHY AM HAVING PAIN DURING SEX

* KITABU CHA UPENDO WA KWELI - TRUE❤️LOVE

* KITABU CHA NDOA - MARRIAGE BOOK

* NAMNA YA KUJUA PENZI LA KWELI - HOW TO KNOW A TRUE❤️LOVE

* NINAISHI KATIKA KARNE TOFAUTI KATIKA MUDA MMOJA - I LIVE IN DIFFERENT CENTURIES AT THE SAME TIME ( A Poem Of Embrooos Lamentations).

* The Books Of Law. Book 1 - 6

πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡

GO TO The link below to discover those books and other good material.

πŸ‘‰ Check Emb Store

☝️☝️Click Link hii kupata vitabu na πŸ™Makala mbalimbali


Written By 

Mr Ambrose Nyoni. The Author.


Comments

Popular Posts